|
Harusi za kizanzibari |
Tangu zamani, kumekuwa na namna tofauti za kusherehekea harusi.mengi kati ya hayo huwa yamerithiwa kutoka kwa mababu na hata yale yanayoitwa kwenda na wakati. Hebu angalia hii;
|
bibi akifanya matani | | | | | | |
|
|
|
Haya ni ya kawaida sana, ni sehemu ya furaha ya wanajamii. Dini nayo ina mafundisho yake katika jambo kama hili. Ni sunna kuvaa vizuri. Mara nyingi jamii ya waislamu hupenda kuvaa kama kanzu aina ya joho na kilemba.
|
vazi la bwana harusi |
Kwa kawaida bwana harusi huwa na wapambe wake ambao huvaa vazi sare ambao huwa linafanana. Baada ya hapo huwa na sehemu muhimu ambayo ni maalumu kwa bwana harusi hao.
|
sehemu mahususi kwa bwana harusi na wapambe wake |
Bwana harusi hukaa juu ya mto na wale wapambe wake hukaa ama juu ya mkeka wa asili au busati safi la kupendeza. Mbele yao huwekwa kinara ambacho ndani yake huwa na mrashi, tende, biskuti, pelemende na hata wakati mwengine sigara.
Baada ya hapo hatua za kuozeshwa huanza. Baba wa biharusi ndie anaekuwa na haki na mamlaka ya kumuozesha binti yake. Kwa taratibu za kiislamu kama baba adharurika au kufariki, anaepaswa kumuozesha binti huyo ni babu, kaka au baba mdogo wa harusi.
No comments:
Post a Comment